UMOJA WA MATAIFA OFISI YA IDARA YA HABARI TAARIFA YA
ULIMWENGU JUU YA HAKI ZA BINADAMU |
UNIVERSAL DECLARATION
OF HUMAN RIGHTS |
Utangulizi
Kwa kuwa kukiri heshima ya asili na haki sawa na binadamu wote ndio
msingi wa uhuru, haki na amani duniani, |
Preamble
Whereas recognition of the inherent dignity and of the equal and
inalienable rights of all members of the human family is the foundation of freedom,
justice and peace in the world, |
Kwa kuwa
kutojali na kudharau haki za binadamu kumeletea vitendo vya kishenzi ambavyo vimeharibu
dhamiri ya binadamu na kwa sababu taarifa ya ulimwengu ambayo itawafanya binadamu
wafurahie uhuru wao wa kusema, kusadiki na wa kutoogopa cho chote imekwisha kutangazwa
kwamba ndio hamu kuu ya watu wote, |
Whereas
disregard and contempt for human rights have resulted in barbarous acts which have
outraged the conscience of mankind, and the advent of a world in which human beings shall
enjoy freedom of speech and belief and freedom from fear and want has been proclaimed as
the highest aspiration of the common people, |
Kwa kuwa
ni lazima, ili mtu asishurutizwe kuomba msaada kutokana na maasi ya kupinga dhuluma na
uonevu, kwamba haki za binadamu ziwe chini ya ulinzi wa sheria, |
Whereas
it is essential, if man is not to be compelled to have recourse, as a last resort, to
rebellion against tyranny and oppression, that human rights should be protected by the
rule of law, |
Kwa kuwa
ni lazima kabisa kuendeleza uhusiano wa kirafiki kati ya mataifa, |
Whereas
it is essential to promote the development of friendly relations between nations, |
Kwa kuwa
watu wa Umoja wa Mataifa wamethibitisha tena katika Mkataba wao imani yao katika haki za
asili, heshima na thamani ya binadamu na katika usawa wa haki kwa wanaume na wanawake, na
kwa sababu wamekata shauri la kuendeleza mambo ya starehe na hali bora za maisha ya watu
kwa kuwa na uhuru zaidi, |
Whereas
the peoples of the United Nations have in the Charter reaffirmed their faith in
fundamental human rights, in the dignity and worth of the human person and in the equal
rights of men and women and have determined to promote social progress and better
standards of life in larger freedom, |
Kwa kuwa
Nchi zilizo Wanachama zimeahidi, kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa, kukuza na kuheshimu
haki za binadamu na uhuru wake wa asili, |
Whereas
Member States have pledged themselves to achieve, in cooperation with the United Nations,
the promotion of universal respect for and observance of human rights and fundamental
freedoms, |
Kwa kuwa
kuzitambua haki hizi na uhuru huu ni jambo la maana sana kua kutimiza ahadi hiyo,
Kwa hiyo basi, |
Whereas
a common understanding of these rights and freedoms is of the greatest importance for the
full realization of this pledge, Now, therefore, |
Baraza Kuu
linatangaza Taarifa Hii Ya Ulimwengu Juu Ya Haki Za Binadamu
kama ndio nguzo ya juhudi kwa watu wa mataifa yote ambayo hatimaye kila mtu na kila jamii
ya watu - kwa kushikilia daima Taarifa hiyo - watajitahidi kufundisha jinsi ya kukuza
heshima ya haki hizo na uhuru huo. Na mataifa yote yatajitahidi kuzifanya haki hizo
zifahamike miongoni mwa Nchi zilizo Wanachama na miongoni mwa watu zinaowatawala. |
The
General Assembly, proclaims this
Universal Declaration of Human Rights as a common standard of achievement for all peoples
and all nations, to the end that every individual and every organ of society, keeping this
Declaration constantly in mind, shall strive by teaching and education to promote respect
for these rights and freedoms and by progressive measures, national and international, to
secure their universal and effective recognition and observance, both among the peoples of
Member States themselves and among the peoples of territories under their jurisdiction. |
Kifungu
cha 1.
Watu wote wamezaliwa huru, hadhi na haki zao ni sawa. Wote
wamejaliwa akili na dhamiri, hivyo yapasa watendeane kindugu. |
Article
1
All human beings are born free and equal in dignity and rights. They
are endowed with reason and conscience and should act towards one another in a spirit of
brotherhood. |
Kifungu
cha 2.
Kila mtu anastahili kuwa na haki zote na uhuru wote ambao umeelezwa
katika Taarifa hii bila ubaguzi wo wote. Yaani bila kubaguana kwa rangi, taifa, wanaume
kwa wanawake, dini, siasa, fikara, asili ya taifa la mtu, mali, kwa kizazi au kwa hali
nyingine yo yote.
Juu ya hayo usifanye ubaguzi kwa kutegemea siasa, utawala au kwa
kutegemea uhusiano wa nchi fulani na mataifa mengine au nchi ya asili ya mtu, haidhuru
nchi hiyo iwe inayojitawala, ya udhamini, isiyojitawala au inayotawaliwa na nchi nyingine
kwa hali ya namna yo yote. |
Article
2
Everyone is entitled to all the rights and freedoms set forth in
this Declaration, without distinction of any kind, such as race, colour, sex, language,
religion, political or other opinion, national or social origin, property, birth or other
status.
Furthermore, no distinction shall be made on the basis of the political, jurisdictional or
international status of the country or territory to which a person belongs, whether it be
independent, trust, non-self-governing or under any other limitation of sovereignty. |
Kifungu
cha 3.
Kila mtu ana haki ya kuishi, haki ya uhuru, na haki ya kulindwa
nafsi yake. |
Article
3
Everyone has the right to life, liberty and security of person. |
Kifungu
cha 4.
Mtu ye yote asifanywe mtumwa au mtwana; utumwa na biashara yake ni
marufuku kwa kila hali. |
Article
4
No one shall be held in slavery or servitude; slavery and the slave
trade shall be prohibited in all their forms. |
Kifungu
cha 5.
Mtu ye yote asiteswe, asiadhibiwe, asidharauliwe au kutendewa
kinyama au kikatili. |
Article
5
No one shall be subjected to torture or to cruel, inhuman or
degrading treatment or punishment. |
Kifungu
cha 6.
Mbele ya sheria kila mtu ana haki ya kutambulika kama mtu. |
Article
6
Everyone has the right to recognition everywhere as a person before
the law. |
Kufungu
cha 7.
Mbele ya sheria watu wote ni sawa na wanastahili haki sawa za
kulindwa. Wote wana haki sawa ya kulindwa kutokana na ubaguzi wo wote unaoweza kuvunja
Taarifa hii na mambo yo yote yanayoweza kuleta ubaguzi kama huo. |
Article
7
All are equal before the law and are entitled without any
discrimination to equal protection of the law. All are entitled to equal protection
against any discrimination in violation of this Declaration and against any incitement to
such discrimination. |
Kifungu
cha 8.
Kila mtu ana haki ya kutetewa na baraza la hukumu kwa makosa ya
kuvunjiwa haki zake za asili anazostahili kwa mujibu wa kanuni na sheria. |
Article
8
Everyone has the right to an effective remedy by the competent
national tribunals for acts violating the fundamental rights granted him by the
constitution or by law. |
Kifungu
cha 9.
Mtu ye yote asikamatwe, asifungiwe au kuhamishwa kutoka nchi yake
bila sheria. |
Article
9
No one shall be subjected to arbitrary arrest, detention or exile. |
Kifungu
cha 10
Kila mtu ana haki kamili ya kuhukumiwa vyema hadharani na baraza la
hukumu lililo huru na lisilo na upendeleo katika kutoa uamuzi wa haki zake na wajibu wake
na wa makosa yo yote yanayomhusu. |
Article
10
Everyone is entitled in full equality to a fair and public hearing
by an independent and impartial tribunal, in the determination of his rights and
obligations and of any criminal charge against him. |
Kifungu
cha 11.
- Kila mtu anaeshtakiwa kwa kosa la kuvunja sheria ana haki ya
kuangaliwa kama si mkosefu mpaka imethibitishwe kwa sheria, kwa kuhukumiwa hadharani,
kwamba ana hatia.
- Mtu ye yote asitiwe hatiani kwa tendo lo lote au jambo lo lote ambalo
halikupinga sheria ya taifa au ya kati ya mataifa wakati alipolitenda. Wala asipewe adhabu
kali zaidi kuliko ile iliyokuwamo katika sheria wakati alipofanya kosa.
|
Article
11
- Everyone charged with a penal offence has the right to be presumed
innocent until proved guilty according to law in a public trial at which he has had all
the guarantees necessary for his defence.
- No one shall be held guilty of any penal offence on account of any
act or omission which did not constitute a penal offence, under national or international
law, at the time when it was committed. Nor shall a heavier penalty be imposed than the
one that was applicable at the time the penal offence was committed.
|
Kifungu
cha 12.
Kila mtu asiingiliwe bila sheria katika mambo yake ya faragha, ya
jamaa yake, ya nyumbani mwake au ya barua zake. Wala asivunjiwe heshima na sifa yake. Kila
mmoja ana haki ya kulindwa na sheria kutokana na pingamizi au mambo kama hayo. |
Article
12
No one shall be subjected to arbitrary interference with his
privacy, family, home or correspondence, nor to attacks upon his honour and reputation.
Everyone has the right to the protection of the law against such interference or attacks. |
Kifungu
cha 13.
- Kila mtu ana haki ya kwenda mahali anapotaka na kuishi katika kila
nchi.
- Kila mmoja ana haki ya kuhama kutoka nchi yo yote, hata nchi yake
mwenyewe, na ana haki ya kurejea katika nchi yake.
|
Article
13
- Everyone has the right to freedom of movement and residence within
the borders of each State.
- Everyone has the right to leave any country, including his own, and
to return to his country.
|
Kifungu
cha 14.
- Kila mtu ana haki ya kukimbilia na kustarehe katika nchi nyingine kwa
ajili ya kuepukana na udhalimu.
- Haki hii haiwezi kuombwa kwa udhalimu ambao hautokani na makosa ya
mambo ya siasa au na makosa ya maazimio na kanuni za Umoja wa Mataifa.
|
Article
14
- Everyone has the right to seek and to enjoy in other countries asylum
from persecution.
- This right may not be invoked in the case of prosecutions genuinely
arising from non-political crimes or from acts contrary to the purposes and principles of
the United Nations.
|
Kifungu
cha 15.
- Kila mtu ana haki ya utaifa.
- Mtu ye yote asinyang'anywe utaifa wake bila sheria wala asinyimwe
haki ya kujibadili taifa lake kama akitaka.
|
Article
15
- Everyone has the right to a nationality.
- No one shall be arbitrarily deprived of his nationality nor denied
the right to change his nationality.
|
Kifungu
cha 16.
- Watu wazima, wanaume kwa wanawake wana haki ya kuoana na kuunda jamaa
bila kizuio cho chote kwa sababu ya rangi, taifa au dini. Wana haki sawa za ndoa wakati wa
maisha yao ya ndoa na wakati wa kutenguka ndoa.
- Ndoa inaweza kufungwa tu kwa hiari na mapatano kamili kati ya hao
wanaotaka kuoana.
- Jamaa ni kiungo cha asili cha jamii ya watu, na inastahili kulindwa
na watu pamoja na Serikali.
|
Article
16
- Men and women of full age, without any limitation due to race,
nationality or religion, have the right to marry and to found a family. They are entitled
to equal rights as to marriage, during marriage and at its dissolution.
- Marriage shall be entered into only with the free and full consent of
the intending spouses.
- The family is the natural and fundamental group unit of society and
is entitled to protection by society and the State.
|
Kifungu
cha 17.
- Kila mtu ana haki ya kuwa na mali yake binafsi au kwa kushirikiana na
watu wengine.
- Mtu asinyang'anywe mali yake bila sheria.
|
Article
17
- Everyone has the right to own property alone as well as in
association with others.
- No one shall be arbitrarily deprived of his property.
|
Kifungu
cha 18.
Kila mtu ana haki ya uhuru wa mawazo, dhamira na dini; haki hii
inahusu pia uhuru wa kubadili dini yake au imani, na uhuru wa kubainisha hadharani au
faraghani-akiwa peke yake au na watu wengine-dini yake kwa kufundisha, kwa vitendo,
kuabudu na kwa kuadhimisha. |
Article
18
Everyone has the right to freedom of thought, conscience and
religion; this right includes freedom to change his religion or belief, and freedom,
either alone or in community with others and in public or private, to manifest his
religion or belief in teaching, practice, worship and observance. |
Kifungu
cha 19.
Kila mmoja ana haki ya uhuru wa kutoa na kueleza maoni yake; haki
hii inahusu pia uhuru wa kushikilia maoni yake bila kuingiliwa kati, na uhuru wa kutafuta
na kutoa habari na maoni kwa njia yo yote bila kujali mipaka. |
Article
19
Everyone has the right to freedom of opinion and expression; this
right includes freedom to hold opinions without interference and to seek, receive and
impart information and ideas through any media and regardless of frontiers. |
Kifungu
cha 20.
- Kila mtu anayo haki ya kushiriki katika mkutano na chama kwa hali ya
amani.
- Mtu ye yote asilazimishwe kuwa manachama wa chama fulani.
|
Article
20
- Everyone has the right to freedom of peaceful assembly and
association.
- No one may be compelled to belong to an association.
|
Kifungu
cha 21.
- Kila mmoja anayo haki ya kushiriki katika Serikali ya nchi yake yeye
mwenyewe binafsi au kwa njia ya mjumbe aliemchagua kwa hiari yake.
- Kila mmoja anayo haki sawa ya kufanya kazi katika Serikali; matakwa
hayo huonyeshwa katika uchaguzi halisi unaofanywa muda baada ya muda ambao kila mtu hupiga
kura na ambao hufanywa kwa kura ya siri na kila mtu kwa hiari yake.
- [Article 21.3 is not available]
|
Article
21
- Everyone has the right to take part in the government of his country,
directly or through freely chosen representatives.
- Everyone has the right to equal access to public service in his
country.
- The will of the people shall be the basis of the authority of
government; this will shall be expressed in periodic and genuine elections which shall be
by universal and equal suffrage and shall be held by secret vote or by equivalent free
voting procedures.
|
Kifungu
cha 22
Kila mtu, kama raia, anayo haki ya kutunzwa na anastahili kupata
hali zinazotokana na uchumi, starehe na utamaduni-ambazo ni za lazima kwa hali bora na
maendeleo ya nafsi yake- kwa njia ya juhudi ya taifa na ushirikiano kati ya mataifa na kwa
mujibu wa utaratibu na utajiri wa kila nchi. |
Article
22
Everyone, as a member of society, has the right to social security
and is entitled to realization, through national effort and international co-operation and
in accordance with the organization and resources of each State, of the economic, social
and cultural rights indispensable for his dignity and the free development of his
personality. |
Kifungu
ch 23.
- Kila mtu ana haki ya kufanya kazi, ya kuchagua kazi aipendayo, ya
kuchagua kazi yenye masharti mazuri na ana haki ya kulindwa asikose kazi.
- Kila mtu ana haki ya kupata mshahara sawa na wengine wenye kazi ya
namna moja bila ubaguzi.
- Kila mfanya kazi anayo haki ya kupata mshahara wa kufaa na
unaopendeza utakao mwezesha yeye mwenyewe pamoja na jamaa yake kuishi katika hali bora, na
ahifadhiwe-ikiwa lazima- maisha yake kwa njia nyingine.
- Kila mtu anayo haki ya kuunda au kujiunga na chama cho chote cha
wafanya kazi kwa ajili ya kulinda haki zake za kazi.
|
Article
23
- Everyone has the right to work, to free choice of employment, to just
and favourable conditions of work and to protection against unemployment.
- Everyone, without any discrimination, has the right to equal pay for
equal work.
- Everyone who works has the right to just and favourable remuneration
ensuring for himself and his family an existence worthy of human dignity, and
supplemented, if necessary, by other means of social protection.
- Everyone has the right to form and to join trade unions for the
protection of his interests.
|
Kifungu
cha 24
Kila mtu ana haki ya kupumzika na kufanya kazi kwa kiasi cha saa
zinazostahili. Pia ana haki ya kupata likizo, kwa vipindi, na kupokea mshahara kama vile
angekuwa kazini. |
Article
24
Everyone has the right to rest and leisure, including reasonable
limitation of working hours and periodic holidays with pay. |
Kifungu
cha 25.
- Kila mtu anayo haki ya kupata hali bora ya maisha yeye mwenyewe
pamoja na jamaa yake na kupata chakula, mavazi, nyumba, matibabu na hifadhi za lazima kwa
maisha yake. Pia ana haki ya kutunzwa wakati wa kazi, wakati wa ugonjwa, wa kutojiweza,
ujane, uzee au anapokosa ridhiki yake kwa kutoweza kujisaidia.
- Akina mama na watoto wanastahili kutunzwa na kupewa msaada maalum.
Watoto wote- wawe wamezaliwa katika hali ya ndoa ama hapana- lazima watunzwe vyema.
|
Article
25
- Everyone has the right to a standard of living adequate for the
health and well-being of himself and of his family, including food, clothing, housing and
medical care and necessary social services, and the right to security in the event of
unemployment, sickness, disability, widowhood, old age or other lack of livelihood in
circumstances beyond his control.
- Motherhood and childhood are entitled to special care and assistance.
All children, whether born in or out of wedlock, shall enjoy the same social protection.
|
Kifungu
cha 26.
- Kila mtu ana haki ya kuelimishwa. Elimu yapasa itolewe bure hasa ile
ya madarasa ya chini. Elimu ya masarasa ya chini ihudhuriwe kwa lazima. Elimu ya ufundi na
ustadi iwe wazi kwa wote. Na elimu ya juu iwe wazi kwa wote kwa kutegemea sifa ya mtu.
- Elimu itolewe kwa madhumuni ya kuendeleza barabara hali ya binadamu,
na kwa shabaha ya kukuza haki za binadamu na uhuru wake wa asili. Elimu ni wajibu ikuze
hali ya kueleana, kuvumiliana na ya urafiki kati ya mataifa na kati ya watu wa rangi na
dini mbali-mbali.Kadhalika ni wajibu iendeleze shughuli za Umoja wa Mataifa za kudumisha
amani.
- Ni haki ya wazazi kuchagua aina ya elimu ya kufunzwa watoto wao.
|
Article
26
- Everyone has the right to education. Education shall be free, at
least in the elementary and fundamental stages. Elementary education shall be compulsory.
Technical and professional education shall be made generally available and higher
education shall be equally accessible to all on the basis of merit.
- Education shall be directed to the full development of the human
personality and to the strengthening of respect for human rights and fundamental freedoms.
It shall promote understanding, tolerance and friendship among all nations, racial or
religious groups, and shall further the activities of the United Nations for the
maintenance of peace.
- Parents have a prior right to choose the kind of education that shall
be given to their children.
|
Kifungu
cha 27.
- Kila mtu anayo haki ya kushiriki katika maisha ya utamaduni ya jamii
yo yote, na ana haki ya kufurahia ustadi wa kazi na kushiriki katika maendeleo ya mambo ya
sayansi na faida zinazotokana nayo.
- Kila mtu ana haki ya kulindwa kwa kila hali kutokana na mambo ya
sayansi aliyoandika, aliyochora au aliyogundua.
|
Article
27
- Everyone has the right freely to participate in the cultural life of
the community, to enjoy the arts and to share in scientific advancement and its benefits.
- Everyone has the right to the protection of the moral and material
interests resulting from any scientific, literary or artistic production of which he is
the author.
|
Kifungu
cha 28.
Ni haki kila mtu alindwe na taratibu au kanuni za jamii na
zinazohusu mataifa mbalimbali ambazo ndani yake uhuru na haki zilizoelezwa katika Taarifa
hii zinaweza kuhifadhiwa barabara. |
Article
28
Everyone is entitled to a social and international order in which
the rights and freedoms set forth in this Declaration can be fully realized. |
Kifungu
cha 29.
- Kila mtu ana wajibu kwa watu wa jamii yo yote ambao kati yao tu ndio
yanaweza kupatikana maendeleo kamili ya hali bora ya maisha yake.
- Katika kutumia haki na uhuru wake, kila mtu itambidi kufuata kanuni
zile tu zilizowekwa na sheria kwa ajili ya kulinda heshima inayotakiwa juu ya haki na
uhuru wa watu wengine, na kwa ajili ya kuhifadhi kanuni za haki, usalama na hali njema ya
maisha katika jamii ya kidemokrasi.
- Uhuru huu na haki hizi kamwe visitumiwe kinyume cha maazimio na
kanuni za Umoja wa Mataifa.
|
Article
29
- Everyone has duties to the community in which alone the free and full
development of his personality is possible.
- In the exercise of his rights and freedoms, everyone shall be subject
only to such limitations as are determined by law solely for the purpose of securing due
recognition and respect for the rights and freedoms of others and of meeting the just
requirements of morality, public order and the general welfare in a democratic society.
- These rights and freedoms may in no case be exercised contrary to the
purposes and principles of the United Nations.
|
Kifungu
cha 30.
Hakuna maneno yo yote katika Taarifa hii yanayoweza kubashiriwa
kwamba yanaruhusu nchi yo yote, kikundi cha watu au mtu fulani kufanya au kushughulika na
jambo lo lote ambalo nia yake ni kuharibu uhuru haki zilizoelezwa humu. |
Article
30
Nothing in this Declaration may be interpreted as implying for any
State, group or person any right to engage in any activity or to perform any act aimed at
the destruction of any of the rights and freedoms set forth herein. |